YESU NAKUPENDA (By: F Tumaini Swai)
Ee Yesu natamani uwe wangu siku zote,
Na mimi niishinawe niwe wako milele X2
(Kweli) Yesu nakupenda (Ingia) mwangu unilinde,
Nijalie Bwana wangu nikupende siku zote.x2
Ee Yesu unijaze katika Ekaristia niweze kuvishinda
Vishawishi vyake shetani.
Unitakase Yesu, kwa mwiliyo na damuyo nioshe
Niwe safi, niziepuke tamaa mbaya.
Mwokozi nakupenda, njoo Yesu niishi nawe,
Nijalie Bwana wangu, nilidumishe pendo langu.
Unijalie Yesu nilijue neno lako,
nilitangaze kwa watu wote wa Dunia.
Unipe ujasiri, wakukuhubiri wewe,
Niyafanye mataifa yote yakufuate wewe.
ENGLISH TRANSILATION:
Oh Jesus, I want you to be mine always,
And let me be yours forever X2
(True) Jesus I love you (Enter) my heart protect me,
Grant me my Lord that I may love you always.x2
O Jesus, fill me in the Eucharist so I can overcome them
His temptations the devil.
Cleanse me Jesus, wash my body with your blood
Let me be pure, let me avoid bad desires.
Savior I love you, come Jesus let me live with you,
Grant me my Lord, keep my love.
Grant me Jesus that I may know your word,
I announce it to all the people of the Earth.
Give me courage, when I preach your word,
Make all nations follow you.