S4 Kiswahili
S4 Kiswahili
and Sports
HOME-STUDY
I O
N
4
R
S E
Published 2020
This material has been developed as a home-study intervention for schools during the
lockdown caused by the COVID-19 pandemic to support continuity of learning.
Therefore, this material is restricted from being reproduced for any commercial gains.
FOREWORD
The COVID-19 outbreak and subsequent closure of all has had drastically
impacted on learning especially curriculum coverage, loss of interest in
education and learner readiness in case schools open. This could result in
massive rates of learner dropouts due to unwanted pregnancies and lack
of school fees among others.
Alex Kakooza
Permanent Secretary
Ministry of Education and Sports
iii
ACKNOWLEDGEMENTS
The Centre appreciates the contribution from all those who guided
the development of these materials to make sure they are of quality;
Development partners - SESIL, Save the Children and UNICEF; all the
Panel members of the various subjects; sister institutions - UNEB and DES
for their valuable contributions.
Grace K. Baguma
Director,
National Curriculum Development Centre
iv
SELF-STUDY LEARNING
Dear learner, you are welcome to this home-study package. This content
focuses on critical competences in the syllabus.
The content is organised into lesson units. Each unit has lesson activities,
summary notes and assessment activities. Some lessons have projects
that you need to carry out at home during this period. You are free to use
other reference materials to get more information for specific topics.
The content has been developed with full awareness of the home learning
environment without direct supervision of the teacher. The methods,
examples and activities used in the materials have been carefully selected
to facilitate continuity of learning.
You are therefore in charge of your own learning. You need to give
yourself favourable time for learning. This material can as well be used
beyond the home-study situation. Keep it for reference anytime.
Enjoy learning
v
SELF-STUDY LEARNING
Term 2&3
Kiswahili Self-study Material Kidato cha nne
Utangulizi
Je, unajua kuwa kunyambua kitenzi ni kuzalisha neno au maneno mapya? Umeshawahi
kunyambua vitenzi vya Kiswahili na kuzalisha maneno mapya kutokana na vile vitenzi vya
awali? Katika somo hili utajifunza kuhusu hali mbalimbali za mnyambuliko wa vitenzi.
Maagizo: Tafuta pahali mwafaka kusoma makala haya. Utafanya mazoezi na shughuli zote
zilizomo. Kumbuka kuwa baadhi ya shughuli zinaweza kuchukua muda mrefu. Soma maagizo
kwa makini kabla ya kufanya zoezi/shughuli husika.
Mnyambuliko wa vitenzi
Vitenzi huwa katika hali/kauli mbalimbali kama zinavyooneshwa hapo chini:
Shughuli 1.1: Kutambua hali za mnyambuliko wa vitenzi
1. Soma kwa sauti na kisha utafakari juu ya hali/kauli zinazooneshwa hapo chini.
2. Taja vitenzi ambavyo vimenyambuliwa katika hali/kauli zifuatazo.
Hali ya kutenda
Inahusisha upande mmoja k.m;
Ninasoma kitabu.
Hali ya kutendea/kufanyia
Hii inahusisha pande mbili ambapo upande mmoja unafanya jambo kwa upande mwingine.
K.m; Mama anapigia baba simu.
Hali ya kutendewa
Katika kauli hii, upande mmoja unatenda jambo kwangu au kwa mtu mwingine. K.m;
Nimepigiwa simu au Baba atapigiwa simu.
1
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Hali ya kutendesha
Hii ni hali ya kusababisha jambo litendeke. K.m Mama anamlisha mtoto. Hapa mama
anamfanya mtoto ale chakula.
Hali ya kutendana
Hapa upande mmoja unatenda na wa pili pia unatenda. Kwa hivyo wanatendana. Hali
ya kutendana ni pale ambapo mtu au mnyama humtendea mwingine kitendo kilekile ali-
chotendewa K.m; Ninampenda naye ananipenda –Tunapendana.
Hali ya kutendeana
Katika hali hii, watu wanafanyiziana vitendo. Kwa mfano, Akello akimpigia simu Chemu-
tai naye Chemutai akampigia simu Akello, watakuwa wanapigiana simu.
Hali ya kutendatenda
Hii ni hali ya kurudiarudia kitendo mara kwa mara. K.m; Tangu Virusi vya Korona viingie
nchini Uganda, watu wananawanawa mikono yao.
Hali ya kutendeka
Hapa jambo linatokea labda bila kuingiliwa na upande wowote.k.m; Kitabu kimeanguka.
Au Msichana huyu alirembeka.
2
SELF-STUDY LEARNING
Muhtasari wa mada
Je, unakumbuka kuwa katika mada hii umejifunza kuhusu, kunyambua vitenzi katika hali
ya kutenda, kutendea, kutendewa, kutendesha, kutendeana na kutendana, kutendaten-
da na kutendeka? Ujuzi huu utakusaidia kuimarisha umilisi wako wa lugha ya Kiswahili.
Utangulizi
Unajua kuwa wanafunzi wengi hawafanyi vizuri sana katika kujibu maswali ya ufahamu?
Tatizo hili hutokana na ukosefu wa makini wakati wa kusoma ufahamu na hata wakati wa
kuyajibu maswali yenyewe. Je, wewe kama mtahiniwa unafaa kufanya yapi ili ufanye vizuri
katika sehemu ya ufahamu? Katika somo hili utajifunza kanuni mbalimbali unazostahili
kufuata ili ufue dafu katika ufahamu.
Maagizo: Tafuta pahali mwafaka kusoma makala haya. Utafanya mazoezi na shughuli zote
zilizomo. Kumbuka kuwa baadhi ya shughuli zinaweza kuchukua muda mrefu. Soma maagizo
kwa makini kabla ya kufanya zoezi/shughuli husika.
3
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Ufahamu
1. Soma kanuni au utaratibu ufuatao ili uweze kumakinika katika kujibu maswali ya
ufahamu.
Utaratibu wa ufahamu
4
SELF-STUDY LEARNING
Muhtasari wa mada
Je, unakumbuka kuwa katika mada hii umejifunza kuhusu, kusoma makala mbalimbali ya
ufahamu na kujibu maswali? Ujuzi huu utaimarisha uelewa wako wa lugha ya Kiswahili.
Umilisi:
Utangulizi
Unajua kuwa ili mwanafunzi aweze kuandika insha nzuri, sharti aelewe na kufuata sheria za
uandishi wa insha? Je, unajua kuwa wanafunzi wengi hufanya makosa katika uandishi wa
insha bila kujua? Katika somo hili utajifunza kanuni mbalimbali unazostahili kufuata katika
uandishi insha nzuri ili kuepuka kufanya makosa.
Maagizo: Tafuta pahali mwafaka kusoma makala haya. Utafanya mazoezi na shughuli zote
zilizomo. Kumbuka kuwa baadhi ya shughuli zinaweza kuchukua muda mrefu. Soma maagizo
kwa makini kabla ya kufanya zoezi/shughuli husika.
5
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Uandishi wa Insha
Kuna aina nyingi za insha ambazo mwanafunzi wa kidato cha nne anatakiwa kuandika.
Ili uweze kuandika insha hizo vizuri, sharti uelewe na uzifuate sheria za utunzi wa insha.
Ulikuwa unajua?
Wanafunzi wengi hufanya makosa katika uandishi wa insha. Yakariri mako-
sa yafuatayo na uyalinganishe na yale unayoyajua :
1. Kutosoma insha mara tu baada ya kuiandika. Ni vizuri kusoma insha ili kuyasahi-
hisha makosa uliyoyafanya wakati wa kuandika.
2. Kutumia maneno usiyokuwa na uhakika kuyahusu. Badala yake, unafaa kuuliza au
kufanya utafiti kuyahusu maneno yale.
3. Kukatakata maneno k.m angesoma, nilipo fika badala ya nilipofika, aliye kuita
badala ya aliyekuita.
4. Kuyashikanisha maneno k.m. Kwasababu badala ya kwa sababu Kwanini badala
ya kwa nini, n.k.
5. Maendelezo mabaya k. minchibadala ya nchi, kua badala ya kuwa, tama badala
ya tamaa, n.k.
6. Kutumia sentensi ndefu na za kuchosha. Mwanafunzi anashauriwa kutumia sen-
tensi fupi na sahihi.
7. Matumizi ya maneno yasiyo ya Kiswahili. Maneno yasiyo ya Kiswahili yatabeba
adhabu kali katika kutuza alama.
8. Matumizi ya maneno ya mkato kama dadangu, mamaye yaepukwe.
Utangulizi
Kufikia kidato cha nne, mwanafunzi anatakiwa kutambua insha mbalimbali ambazo ana-
takiwa kuandika katika mtihani wa taifa. Insha hizo zimegawanywa katika aina mbalim-
bali. Katika somo hili, utajifunza namna ya kuainisha insha mbalimbali.
6
SELF-STUDY LEARNING
Aina za insha
Kufikia kidato cha nne, mwanafunzi anastahili kuwa amejifunza namna ya kuandika in-
sha mbalimbali. Insha hizo ni kama zifuatazo:
a. Insha za mada teule
b. Insha za mwongozo
c. Insha za mjadala
d. Insha za methali mara nyingi hizi huwa chini ya insha za mada teule.
e. Insha za barua
f. Insha za mazungumzo
g. Insha za ratiba
h. Insha za hotuba
i. Insha za kumbukumbu
j. Insha za shajara
k. Insha za picha
l. Insha za ripoti
m. Insha za matangazo
n. Insha za maelekezo, n.k.
Insha hii huhitaji mwanafunzi kutoa hoja za jambo fulani. Katika insha hii, mwanafunzi
anatakiwa kuandika mambo ya ukweli wala si yale ya kubuni. Soma mfano ufuatao wa
insha ya mada teule.
1. Madhara ya ugonjwa wa COVID-19 nchini Uganda.
Utangulizi: Eleza kwa ufupi jinsi ugonjwa wa COVID-19 umekuwa janga kwa taifa la
Uganda.
Mwili: Eleza madhara ya Ugonjwa wa COVID -19. K.m,
-Ugonjwa wa COVID-19 umesababisha watu kupoteza kazi zao
-Watu wameshindwa kukimu mahitaji yao na ya wale wanaowategemea.
-Gharama imeongezeka wa taifa na jamii, k.m, kununua, dawa, vitakasa mikono, bara-
koa, n.k.
-Umaskini kwa kuwa watu hulazimishwa kubaki nyumbani.
-Uchumi huzorota.
-Husababisha vifo, n.k.
7
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Utangulizi
Kuna aina mbalimbali za barua ambazo mwanafunzi wa kidato cha nne anatakiwa ku-
ziandika. Insha hizo za barua ni muhimu sana kwa sababu zinamsaidia mwanafunzi
katika maisha yake ya baadaye. Katika somo hili, utajifunza namna ya kuandika aina
mbalimbali za barua.
Insha ya barua
Kuna aina mbili za barua, yaani; barua ya kirafiki na barua rasmi
Barua ya kirafiki
Hii huandikwa kwa rafiki au hata mtu wa familia. Unaweza kumwandika ndugu au rafiki
yako ili kumjulia hali, kumpongeza, kumpa pole, kumwalika katika sherehe, kumwomba
msaada, n.k.
Barua ya kirafiki huwa na sehemu hizi;
Anwani ya mwandishi, sehemu ya mwandikiwa, utangulizi/aya ya kwanza, mwili/kiwili-
wili, mwisho/tamati na jina la mwandishi.
Ebu soma mfano wa barua ya kirafiki hapo chini:
8
SELF-STUDY LEARNING
Mpendwa baba,
Shikamoo baba! Mimi ni mzima. Natumai pia nyinyi hamjambo huko nyumbani?
Safari yangu kutoka nyumbani hadi Kampala ilikuwa nzuri. Tulisafiri usiku kucha tukaf-
ika asubuhi na mapema.
Shughuli za muhula mpya zimeanza. Masomo ya kidato cha nne ni magumu kiasi lakini
tunajitahidi ipasavyo.
Nimekuandikia barua hii kukuomba pesa za matumizi kwa sababu pesa ambazo ulinipa
nilizitumia kununua vitabu na vifaa vingine vya kutumia hapa shuleni.
Mwanao mpendwa,
Karangwa Zabuloni
Zoezi
Mwandikie rafiki yako barua umweleze jinsi ulivyotumia likizo ya COVID-19.
Barua rasmi
Hizi huandikwa kwa shughuli rasmi au za kiofisi kama vile; kuomba nafasi ya kazi, kuom-
ba nafasi ya masomo, kuomba msamaha, n.k. Barua rasmi ina sehemu zifuatazo; anwani
ya mwandishi-hii hujumuisha makao yake na sanduku la posta (S.L.P), anwani ya mwan-
dikiwa, nani anayeandikiwa kama Kwa Bibi/Bwana, lengo/kichwak.m, KUH: KUOMBA
NAFASI YA KAZI, utangulizi (aya hii huwa fupi), mwili wa barua, tamati (hii ni aya ya
mwisho), jina la mwandishi sanasana huwa hivi:
Wako mwaminifu,
(Sahihi/saini)
Jina
Angalia mfano wa barua rasmi.
9
KISWAHILI | SENIOR FOUR
LUWERO-UGANDA
29. SEPTEMBA.2020
Zoezi
1. Andika barua kwa Mwalimu mkuu ukimwomba nafasi ya kujiunga na kidato cha
tano katika shule yake.
2. Andika barua kwa mwalimu ukimwomba msamaha kwa kutohudhuria masomo bila
kumjulisha mapema.
10
SELF-STUDY LEARNING
Utangulizi
Kuna aina mbalimbali za ripoti ambazo mwanafunzi wa kidato cha nne anatakiwa
kuziandika. Ripoti hizo ni muhimu sana kwa sababu zinamsaidia mwanafunzi katika
maisha yake ya baadaye. Katika somo hili, utajifunza namna ya kuandika ripoti.
Uandishi wa ripoti
Ripoti ni rekodi inayotolewa kama taarifa juu ya mtu, kitu au tukio fulani ambalo lime-
tokea, kwa mfano ajali, kifo,ziara, janga au maafa mengine.
Ripoti huandikwa kwa madhumuni ya kutoa taarifa ili taarifa hiyo iweze kufanyiwa kazi
au walau kuhifadhiwa kama kumbukumbu.
Muundo wa ripoti
1. Kichwa cha ripoti/mada/anwani. Ripoti lazima iwe na kichwa cha habari; kichwa
hicho huandikwa kwa maneno machache. Mambo muhimu yanayotakiwa kuwepo katika
kichwa cha ripoti ni:
• Mahali pa tukio
• Aina ya tukio
• Tarehe ya tukio
• Muda wa tukio
3. Kiini cha ripoti/mwili. Kiini cha ripoti kina maelezo yote kuhusiana na tukio lenyewe.
Sehemu hii huelezea kwa ufasaha mambo yaliyotokea, chanzo chake, ukubwa wake, wa-
husika, na tukio linalohusika.
4. Mwisho wa ripoti. Hii ni sehemu ya mwisho ya ripoti. Sehemu hii huonesha mambo
makuu mawili:
11
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Utangulizi
Kuhusu shule
Shule hii kirasmi ainaitwa Shule ya Sekondari ya Kotido. Ilianzishwa mwakani 1987
na sasa ina jumla ya wanafunzi elfu moja mia mbili. Inafundisha wasichana na wavu-
lana. Mwalimu mkuu wa Shule hii anaitwa Bi. Majaliwa Paskali na naibu wake ni Bw.
MashakaMengi. Idadi ya walimu ni sitini na watano na wafanyakazi wengine ni takribani
thelathini. Shule hii inapatikana wilayani Kotido.
12
SELF-STUDY LEARNING
Zoezi
1. Wanafunzi wa shule ya upili ya Kyamaneno wamefanya mgomo mbaya sana na
wamechoma nyumba ya mwalimu mkuu. Walimu mpaka sasa hawajajua chanzo
cha mgomo huo hatari. Afisa wa elimu katika wilaya ya Nakaseke ameteua kamati
ya watu watano na wewe ni katibu wao. Andika ripoti kuhusu chanzo cha mgomo
huo.
2. Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, kumetokea ajali nyingi za barabarani katika
barabara ya kutoka Kampala kuelekea Masaka. Inspekta Mkuu wa polisi ameteua
kamati ya watu watano kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hizo na wewe
ndiye katibu wao. Andika ripoti kuhusu chanzo cha ajali hizo mbaya.
Funzo la tano: Kuandika insha ya kumbumbuku za mkutano
13
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Umilisi:
Baada ya kujifunza somo hili, utaweza kuandika kumbukumbu za mkutano.
Utahitaji vifaa kama: muda, daftari, kalamu, n.k.
Utangulizi
Kumbukumbu za mkutano
14
SELF-STUDY LEARNING
Waliohudhuria
1. Okello Jude - Mwenyekiti
2. Atwine Dilan - Naibu Mwenyekiti
3. Yahaya Mohamed - Mweka Hazina
Waliotoa udhuru
1. Twesiime Richard - Naibu Katibu
2. Kabugho Rita - Mwanachama
3. Mahoro Irene - Mwanachama
Waliokosa kuhudhuria bila udhuru
1. Chesang Betty - Mwanachama
2. Osele Nicho - Mwanachama
Ajenda
1. Kufunguliwa kwa mkutano
2. Kusomwa na kuthibitishwa kwa kumbukumbu za mkutano wa awali
3. Yaliyotokana na kumbukumbu hizo.
4. Miradi ya Chama.
5. Maandalizi ya Kongamano
6. Shughuli nyinginezo.
Mkutano ulifunguliwa kwa maombi saa tano kamili asubuhi. Mwenyekiti aliwashukuru
wanachama kwa kuhudhuria kwao na kuwafahamisha kuwa kulikuwa na mhadhiri mgeni
mlezi wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili, Bi. Asiimwe Phionah. Kisha aliwaomba
wanachama wamuunge mkono ili chama kiendelee.
Kumb: 02/2020 Kusomwa na kuthibitishwa kwa kumbukumbu za mkutano wa awali
Kumbukumbu za mkutano uliotangulia zilizosomwa na katibu Ojok Peter na kuthibitish-
wa na wanachama kuwa zilikuwa rekodi kamili ya mambo yaliyozungumziwa na hivyo
kuidhinishwa na mwenyekiti na katibu wake.
Kumb: 03/2020 Yaliyotokana na kumbukumbu hizo
Kwa kuwa hakukuwa na mengi yaliyotokana na mkutano uliotangulia, katibu aliomba
wanachama waendelee na ajenda za siku.
15
KISWAHILI | SENIOR FOUR
endesha miradi yao. Pia, walikubaliana kuwa wasajili wanachama wengine kumi ili wapa-
te pesa zaidi za kuendesha shughuli za chama. Aidha, walikubaliana kuwa waanzishe
mradi mpya wa kuuza vitabu vya Kiswahili ili wapate kipato zaidi.
Kumb: 05/2020 Maandalizi ya Kongamano
Wanachama walikubaliana kuwa kongamano la Kiswahili la kitaifa lizungumziwe katika
mkutano utakaofuata. Mlezi wa Chama aliungwa mkono wazo hili na hivyo kongamano
litazungumziwa leo.
Kumb: 06/2017 Shughuli nyinginezo
Ilipitishwa kuwa:
(a) kila mwanakamati ashawishi watu watano waingie katika chama
(b) kila mwanachama atafute michango kutoka nje ya chuo ili wapate usaidizi wa kiu-
chumi.
Kumb: 07/2020 Kufungwa kwa mkutano
Kwa kuwa hapakuwa na jingine la ziada, mkutano ulifungwa kwa maombi kutoka kwa
Kayihura Ismael saa saba za mchana.
Thibitisho
Mwenyekiti ………………………. Sahihi …………………… Tarehe
………………… Katibu ………………………… Sahihi …………………….
Tarehe …………………
Zoezi
Wewe ni katibu mkuu wa Chama cha Wazalendo shuleni mwako, ziandike kumbukumbu
za mkutano uliokuwepo tarehe 2 Machi mwaka huu ambao uliuhudhuria. Tumia maneno
yasiyopungua 150 wala kuzidi maneno 250.
16
SELF-STUDY LEARNING
Muhtasari wa mada
Je, unakumbuka kuwa katika mada hii umejifunza kuhusu, kuandika aina mbalimbali za
insha? Ujuzi huu utakusaidia kuimarisha mawasiliano yako katika lugha ya Kiswahili.
Umilisi:
Baada ya kujifunza somo hili utaweza:
i) Kutambua utaratibu wa kufupisha makala.
ii) Kufupisha makala mbalimbali kwa kufuata utaratibu mwafaka.
Utahitaji vifaa kama; muda, daftari, kalamu, n.k
Utangulizi
Je, ulikuwa unajua kuwa neno ufupisho linatokana na neno ‘fupisha’ lililo na maana
ya kupunguza urefu? Katika muktadha wa shuleni, neno ufupisho linamaanisha kutoa
muhtasari wa maudhui husika au taarifa uliyopewa. Katika funzo hili, utajifunza kuhusu
kufupisha makala mbalimbali.
Maagizo: Tafuta pahali mwafaka kusoma makala haya. Utafanya mazoezi na shughuli zote
zilizomo. Kumbuka kuwa baadhi ya shughuli zinaweza kuchukua muda mrefu. Soma maagizo
kwa makini kabla ya kufanya zoezi/shughuli husika.
Ufupisho
Ufupisho ni hali ya kutoa muhtasari wa maudhui ya makala au habari fulani. Kwa mfano
habari yenye aya ishirini au zaidi yaweza kupunguzwa urefu hadi aya moja yenye ma-
neno yasiyozidi mia. Ufupisho siyo tu kupunguza urefu au idadi ya maneno katika ibara
iliyopewa. La hasha! Wakati wa kufupisha, unastahili kutafuta hoja muhimu au maudhui
17
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Mfano;
Fuata utaratibu mwafaka kufupisha aya hii katika maneno yasiyozidi 20.
Ajali ni tukio linalotokea kwa ghafla. Ajali ni kitu kinachotokea bila kupangwa wala
kutarajiwa. Tukio hili aghalabu husababisha madhara au hatari. Waathiriwa wa ajali
hupatwa na matata kama maumivu, kupoteza viungo fulani vya mwili kama mikono, mi-
guu miongoni mwa vingine. Ajali inaweza kutokea wakati mtu anasafiri, akiwa amelala,
akiwa ameketi na katika hali yoyote ile anayekuwemo.
Vidokezo
-Ajali ni tukio la ghafula.
-Hutokea bila kupangwa
-Husababisha madhara/hatari kv; maumivu, kupoteza viungo vya mwili, n.k.
-Ajali hutokea wakati wowote.
Nakala chafu
Ajali ni tukio la kighafula linalotokea bila kupangwa. Ajali husababisha madhara kama
maumivu, kupoteza viungo vya mwili. Ajali inaweza kutokea wakati wa kusafiri, kulala,
kuketi na katika hali yoyote ile.
Nakala safi
18
SELF-STUDY LEARNING
Ajali ni tukio la kighafula. Husababisha madhara kamakupoteza viungo vya mwili. Ajali
inaweza kutokea wakati wowote ule.
(Maneno 18)
Zoezi: Kufupisha makala
1. Fupisha makala yafuatayo kwa maneno 100.
Siku moja punda wa Abunuwas alikuwa na kiu. Kitu cha kumtilia maji apate kunywa hana.
Akaenda kwa jirani yake, akamwambia, niazime sufuria yako nimnyweshee punda wangu
maji. Yule jirani akampa Abunuwas sufuria, akaenda zake. Akakaa nayo siku ya kwanza,
siku ya pili, siku ya tatu. Siku ya nne, akaamua kutwaa ile sufuria kwa mwenyewe, akatia
na kisufuria kidogo ndani, akampelekea mwenyewe.
Abunuwas alipofika kwa jirani yake, akamwambia, sifuria yako ndiyo hii hapa.
Akaitwaa, akaona ndani kisufuria kidogo, akanena, Hiki kisufuria kidogo si chetu.
Abunuwas akanena, mimi si mwizi siwezi kuiba mali ya watu; sufuria yako imezaa kwan-
gu, na huyu mtoto wake. Yule mwenye sufuria akafurahi sana, akanena, Nyumba ya
Abunuwas ina baraka sana, inazaa hata sufuria.
Hata siku ya tatu akaenda kuiazima sufuria ile ile. Akapewa. Na safari hii Abunuwas
akakaa nayo hakuirudisha. Mwenye sufuria akaenda kuuliza kwa Abunuwas sufuria
yake. Abunuwas akanena, sufuria yako imekufa. Yule akanena, Shaba hufa? Abunuwas
akanena, Haikuzaa? Akanena, ilizaa. Abunuwas akanena, Kila kitu kinachozaa, hatima
yake hufa. Akashindwa kumjibu. Akawauliza wanachuoni habari hii, wakamjibu vile vile,
hakika kinachozaa na kufa hakina budi. Abunuwas akahodhi sufuria.
Muhtasari wa mada
Je, unakumbuka kuwa katika mada hii umejifunza kuhusu, kufupisha makala mbalimbali
kwa kuzingatia hoja muhimu. Ujuzi huu utakufaa katika maisha yako ya kila siku.
19
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Umilisi:
Baada ya kujifunza somo hili utaweza:
i) Kutambua utaratibu wa kutafsiri makala.
ii) Kutafsiri makala mbalimbali kwa kufuata utaratibu mwafaka.
Utangulizi
Unajua kuwa tafsiri ni muhimu katika maisha yetu? Tafsiri ni muhimu kwani husaidia ku-
fanikisha mawasiliano, kufanikisha ushirikiano kibiashara, kisiasa, kielemu, kitamaduni
n.k. Aidha tafsiri ni njia ya ajira. Katika somo hili, utajifunza namna ya kutafsiri makala
mbalimbali katika lugha ya Kiswahili.
Maagizo: Tafuta pahali mwafaka kusoma makala haya. Utafanya mazoezi na shughuli zote
zilizomo. Kumbuka kuwa baadhi ya shughuli zinaweza kuchukua muda mrefu. Soma maagizo
kwa makini kabla ya kufanya zoezi/shughuli husika.
Tafsiri
Tafsiri ni shughuli ya kuhamisha mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi
nyingine. Kutafsiri ni kuchukua mawazo yaliyo kwenye maandishi kutoka lugha chanzi
na kuyawasilisha katika lugha lengwa.
Aina za tafsiri
Kuna aina mbalimbali za kufanya tafsiri. Kila aina ina sifa zake, ufaafu wake na upun-
gufu wake.
20
SELF-STUDY LEARNING
Muhtasari wa mada
Je, unakumbuka kuwa katika mada hii umejifunza kuhusu, kutafsiri makala mbalimbali
kutoka kwa lugha ya Kiingereza hadi lugha ya Kiswahili.
21
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Utanguliz
i
Unajua kuwa ni muhimu kujua msamiati wa malipo mbalimbali katika maisha yetu?
Msamiati wa malipo ni muhimusana kwa sababu husaidia kuimarisha mawasiliano yetu
pindi tunapokuwa tunafanya shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi, n.k.
Maagizo: Tafuta pahali mwafaka kusoma makala haya. Utafanya mazoezi na shughuli
zote zilizomo. Kumbuka kuwa baadhi ya shughuli zinaweza kuchukua muda mrefu. Soma
maagizo kwa makini kabla ya kufanya zoezi/shughuli husika.
Malipo
Malipo ni kitu ambacho hutolewa na mtu ili kugharamia shughuli fulani. Malipo pia huit-
wa ada.
22
SELF-STUDY LEARNING
23
KISWAHILI | SENIOR FOUR
Muhtasari wa mada
Je, unakumbuka kuwa katika mada hii umejifunza kuhusu malipo mbalimbali? Msamia-
ti huu wa malipo utakusaidia kuimarisha mawasiliano yako katika lugha ya Kiswahili.
Sherehe
Biashara: Ununuzi na uuzaji wa bidhaa.
Chekechea: shule ya watoto wadogo aghalabu wenye umri usiozidi miaka mitano.
COVID-19: Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Korona. Ulianzia Uchina mwezi
wa Desemba 2019 na kuenea duniani kote. COVID ni kifupi cha Corona
virus Disease na 19 hurejelea mwaka ugonjwa huu ulipozuka yaani 2019.
Kipato: Mavuno au fedha anazopata mtu kutokana na kazi anayoifanya au faida
ya mauzo ya kitu.
Korona: Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
binadamu kuwasiliana.
24
SELF-STUDY LEARNING
Rithi: Pata/miliki kitu kutoka kwa aliyekufa. Akello alirithi mali nyingi.
25
National Curriculum
Development Centre,
P.O. Box 7002,
Kampala.
www.ncdc.go.ug