CHEMBA DISTRICT COUNCIL
STANDARD VII – PRELIMINARY EXAMIMANION
ENGLISH LANGUAGE
SECTION A: (20Marks)
Answer all questions in this section.
1. Listen carefully to the passage read by the invigilator and then answer item (i)-(v) by
choosing the letter of the correct answer and write it in the box provided.
(i) What is the passage about? ( )
A. speakers B. debates C. motion D. arguments E. logic
(ii). How do we call the side which argues against the motion? ( )
A. judge B. Proposing side C. Opposing side D. motion mover E.consensus
(iii) Who declared the winner of the debate? ( )
A. judge B.chairperson C. motion mover D. leader E.a teacher
(iv) should be a neutral person while controllingthedebate ( )
A. motion mover B. timekeeper C.proposers D. Opposers E.chairperson
(v)One of the following is Not the intention of debating? ( )
A. it helps in reasoning logically B.to improve public speaking skills
C. To accept criticism D. to create fear and worries
E. To think critically
2. For each of the items (i) –(v), choose the correct answer and write its letter in the box
provided
i. Mr and Mrs Kilindo slaughtered the cow .............
(A)eacho ther (B) himself (C) themselves (D)herself E) themself
ii. Short time ago Catherine.................... called me.
(A) shall (B) will (C), have (D) has (E) were
iii. It .............. not no rain regularly in Dodoma.
(A) do (B) done (C) does (D)has (E) is
iv. A standard six pupil ............... a letter to her teacher last week
(A) written (B)wrote (C)writes (D) is writing (E) will write
v. Reading books is .................than watching movies
(A) important (B)more important (C)most important
(D) importanter (E)importance
3 Use the sequence markers in the following box to fill in the blanks (i) –(v) in the passage
that follows.
congregation, decade, butchery, before, slowily, catalogue, century
(i)The books were kept on the.................................................................
(ii)At the church we found a large .............................................of worshipers
(iii)We are supposed to wash our hands................................eating anything.
(iv)We can’t wait for him bacause he walks so....................................
(v)Mzee Sangu was born in 1924 and died in 2024.He lived for one.........................
4. Match the words in List A with the corresponding item in list B and write the letter of the
correct answer in the spaces provided
NO LIST A ANSWER LIST B
i. Someone who treats patients A:Jail
ii. The place where criminals are charged by law B:Lawyer
iii. A person who is trained to assist people in legal C:Witness
matters
iv. Something paid illegally to buy your right D:Doctor
v. A person who sees something happening E:Court
F:Corruption
G:Nurse
SECTION B (10 MARKS)
Answe all questions in this section
5.Re - arrange the following sentences to make a meaningfully sentences.
i. He asked me to go to his office to collect our exercise books.
ii. When I was taking rubbish to the dump I saw our English language teacher heading towards his
office.
iii. So I went in to his office and collected our exercise books.
iv. Yesterday I went to school early in the morning.
v. I cleaned our classroom as I was on duty.
i ii iii iv v
SECTION C (20) Marks
6.Complete the following sentences by writing the correct answers.
(i) I have a new bag.The antonym of the underlined word is................
(ii) A bee lives in a hive as a spider lives in a.......................................
(iii) Travelling by air is more expensive............... travelling by train.
(iv) One tooth was paining but the dentist said there where three..............which were decayed.
(v) Words which tell more about verbs or adjectives.................................
7.Read the following passage carefully and answer the following questions that follow by
writing the correct answer in the spaces provided.
I have a dream that I would like to share with you today. My dream job is becoming a Doctor,but how Can
I be courageous enough to go about my fear towards performing surgeries? No,I should be a pilot, but
flying an aeroplane can’t be that easy.How can fly such a big vesselin space? Then,I have to be a
policeman.Oh! Wait! A policeman? Arresting criminals? I think they can hurt me and Iama fraid of a gun.
Then I have to be a teacher. Oh, Yes! I should be the mother of all occupations.
QUESTIONS
(i) What is the passage all about?.......................................................
(ii) What is the speaker’s dream job?.......................
(iii) Which occupation does a speaker think it is the source of all occupations? .....................................
(iv) If the speaker becomes able to fly planes in the space he will ba called..........................
(v) A person who writes poems is called...................................
LISTENING SKILLS
Adebate is the kind of formal discussion on aparticular topic. Adebate involves two sides of which one
Supports the argument. This side is called the proposing side. The other side negates the argument. This is called the
opposing side. The two sides argue logically and they finally reach the consensus. Adebate is always controlled by the
chairperson who is a neutral participant. In the debate there are two secretaries whose role is to records the points of
the speakers. The side that collects many logical points is declared the winners by the Judge. The debates helps to
improve public speaking skills, accepting criticism, reasoning and developing critical thinking skills
MARKING SCHEME
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA
MTIHANI WA KUJIPIMA
SOMO: HISABATI
Muda: Saa 2:00 Januari, 2025
SEHEMU A: (Alama 10)
NA. SWALI KAZI JIBU
a) 6140098+91+81152=
b) 703256 – 596721=
c) 1294×265=
d) 28611÷17=
e) 4 1/3+6 ¼ =
1
f) 15 1/5÷1 1/3=
g) 24.124+20.645=
h) 0.039÷0.3=
i) (-30) – (-21) =
j) (+28) X (-3) =
SEHEMU B: (Alama 30)
a) Tafuta kigawe kidogo cha shirika (KDS) cha 16,
18 na 24
b) Andika dakika 240 katika saa
c) Juma alipeleka kuku 18 sokoni na kila mmoja
alimuuza kwa sh. 25,000. Je, alipata fedha kiasi
gani baada ya mauzo ?
2 d) Mwalimu alinunua machungwa 1600. Baada ya
kuuza 1/8 alibakiwa na machungwa mangapi?
e) Tafuta kigawo kikubwa cha shirika (KKS) cha
19,38 na 57
f) Salome anatakiwa kutafuta jibu la tani 3 kg
9643 g 300×3 Je, ni nini jibu la swali hilo?
a) umri wa Kanankira, Alex, Juma, Janeth, Raheli,
Doto na Asha ni miaka
10, 14, 15, 18, 21, 29, 25, Je, ni umri wa nani ni
namba tasa?
3 b) Andika namba inayofuata katika mfululizo
ufuatao: LXII, LXIV, LXVI, LXVIII ……… kwa kirumi
c)Magdalena alianza kupika saa 6:30 mchana na
kutumia saa mbili na dakika thelathini. Je alimaliza
kupika saa ngapi?
a) Je noti ya sh. 10000 ina sarafu ngapi za shilingi
200?
4
b) Urefu wa barabara ni mita 68,000. Je urefu huo
ni sawa na kilomita ngapi?
c) Iwapo bei ya kilogramu 11 za nyama ni sawa
na shilingi 110,000/= tafuta bei ya kilogramu 6 za
nyama
a) Badili saa 11:00 jioni kuwa mtindo wa saa 24
b) Uzito wa kondoo mmoja ni kilogramu 24 na
gramu 340 Je, uzito wa kondoo 8 wenye uzito
sawa utakuwa ni kilogramu ngapi?
5 c) Laiza alipeleka mbuzi 300 mnadani. Ikiwa mbuzi
20 walipotea na waliobaki walifika mnadani, Je
mbuzi waliofika mnadani wana miguu mingapi?
a) Ikiwa 12 ½ - h =2. Tafuta thamani ya h
b) Jumlisha 14.395+41.395 na kadiria jibu lake
6 katika makumi yaliyo karibu
c) Gari moja husafiri kilomita 7500 kwa saa. Je,
litasafiri km ngapi kwa saa 15?
SEHEMU C: (Alama 10)
7 a) Jedwali hili linaonesha kiasi cha maharage
yaliyovunwa kwa miaka mitano mfululizo:-
mwaka 2013 2014 2015 2016 2017
Uzani(tani) 165 145 250 240 180
Kwa wastani zilivunwa tani ngapi katika miaka mitano?
b) Chakupewa alipewa mshahara wa Shilingi
720,000 na kuutumia kama inavyoonekana
katika kielelezo hapa chini. Je hutumia kiasi
gani kwa chakula?
8
a) Tafuta ukubwa wa pembe y
b) Tafuta mzingo wa umbo hili. Π = 3.14
b) Mche-mraba ufuatao una urefu wa sm 25.
Tafuta eneo la nyuso zake.
MATHEMATICS……MARKING SCHEME
S.N III V VI
1 i Mia tisa tisini na tisa / 10,150 6,221,341
nine hundred and ninety
nine
ii 4763 23232 106,535
iii 4 156 342,910
iv 5001 315 1683
v 1012 11/20 10 7/12
vi 11/30 12 2/3
vii 2/9 44.769
viii 200,010 0.13
ix 36142 -9
x 200 -84
2 i Kujumlisha / 9 KDS 144 / 144 LCM
addition
ii 100 Miaka 12 / 12 years Saa 4 / 4 hrs
iii 101 5 Sh 450,000 / 450,000
shillings
iv 3268 54 Machungwa 1400 /
1400 oranges
v 3636 140,000 KKS 19 / 19 GCF
2 Tani 11 Kg 892 gm 900
/ 11 tone 892 kg
900gm
3 i Sh 700 / 700 shillings 66351 Doto
ii Miti 1436 / 1436 trees Lita 105 / 105 litres LXX
iii 2417 46271 Saa 9:00 alasiri / 3:00
afternoon
iv Miguu 16 / 16 legs
v Duara / circle
4 i Dk 1 / 1 minute Sh 18,000 / 18,000 Sh 50 / 50 shilllings
shillings
ii Mrabaa / square CCV Km 68 / 68 km
iii Pembetatu / triangle THELATHINI NA Sh 60,000 / 60,000
TANO…./ THIRTY shillings
FIVE
iv Mstatili / rectangle
v c
5 i 25 9 1500
ii Mandazi 150 / 150 burns TATU / THREE Kg 194 gm 720 / 194
kg 720 gm
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA
MTIHANI WA UPIMAJI
SOMO: KISWAHILI DARASA: VII.
Muda saa 1:40 Januari 2025
SEHEMU A:
Sikiliza kwa makini habari itakayosomwa na msimamizi, kisha jibu swali 1-5 kwa kuandika
herufi ya jibu sahihi.
1. Vijana wangapi walimvamia mama mashaka?__
(A). Mmoja (B) wanne (C) watatu (D) watano (E). Majuto [ ]
2. Mama Mashaka alimtambua kijana aliyejulikana kwa jina gani?_____
(A) Majuto (B) Matatizo (C) Mtakahela (D) Mashaka (E) Mwizi [ ]
3. Mama mashaka aliibiwa vitu vingapi?__(A). vinne (B). vitatu (C). viwili (D) kimoja (E) Elfu tatu
4. Vijana hao walipewa adhabu gani kutokana na tabia ya wizi waliyonayo?
(A) Kufyeka majani (B) Walifungwa jela (C) walipelekwa polisi (D) walichapwa viboko
(E) Kusafisha ofisi ya kijiji [ ]
5. Ni methali gani inafaa kutokana na Habari uliyosikilia____
(A). Mvumilivu hula mbivu (B) Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwezngu (C) Panya wengi
hawachimbi shimo (D) Ndondondo si chururu (E). Mtaka cha uvunguni sharti ainame [ ]
2. Chagua herufi ya jibu lililosahihi
(i) Mwalimu mkuu alitangaza vita _____ ya watoro shuleni [ ]
(A) Kati (B) Baina (C) Zaidi (D) dhidi (E) Zidi
(ii) Ili kufaulu mtihani…………..kujifunza kwa bidii. [ ]
(A) nibudi (B) hapana budi. (C)kunabudi (D) panabudi (E) Pawe na budi
(iii) Nenda shule haraka. Neno “haraka” limetumika kama nini? [ ]
(A) kitenzi (B) nomino (C) kielezi (D) kisifa (E) kiunganishi
(iv) Shuleni kwetu hakuna mwanafunzi……asiyependa kusoma. [ ]
(A)wowote (B)yeyete (C)yoyote (D)yeyote (E)wote
(v) Hatumkubali…………ana akili nyingi. (A) pamoja (B)ingawa (C) laiti (D)japokuwa (E) labda [ ]
(vi) Alikuwepo lakini nilipofika_____
(A) nilimkuta (B) nilimkuta hayupo (C) sikumkuta (D)nilimkuta ameondoka (E) yote sawa [ ]
(vii) Ungelimuona Daktari juu ya ugonjwa wako … (A) ungalijibiwa (B) ungajibiwa (C) ungelielekezwa
(D) ungalielekezwa (E) ungeelekezwa [ ]
(viii) Neno la jumla la maneno “Meza,Viti,Kabati na kitanda” ni lipi? ….. [ ]
(A) vifaa (B) vyombo vya nyumbani (C) mapambo (D) vifaa vya mbao (E) samani
(ix) Katika neno“Walikimbia”Kiambishi kinachoonesha wakati ni:- ....... [ ]
(A).- mbi- (B).- ki- (C). –li- (D). Wa- (E) - a
(x) “Bata walipigana siku nzima”. Sentensi hii ipo katika kauli ipi?...... [ ]
(A) Kutenda (B). Kutendewa (C). Kutendana (D). Kutendewa (E). Kutendeka
3. Oanisha maneno ya kifungu A na yale ya kifungu B ili kuleta mantiki kwa kaundika herufi ya
jibu sahihi kutoka kifungu B katika mabano uliyopewa
NA KIFUNGU A JAWABU KIFUNGU B
i Ng'ata sikio (i) Kujiremba
ii Kujikwatua (ii) Mchoyo
iii Anika juani (iii) Nong'oneza
iv Mwaga unga (iv) Mroho
v Mkono wa birika (v) Weka hadharani
(vi) Kujichubua
(vii) Kupoteza kazi
4. Jaza nafasi zilizoachwa wazi
(i) Waliimba na kucheza vizuri sana” sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi? _____________________________
(ii) “Masalale!”Tumekwisha, neno masalale limetumika kama aina ipi ya neno? ___________________________
(iii) Mtendega amekuwa Toinyo. Neno Toinyo lina maana gani? _______________________________________
(iv) Tegua kitendawili hiki? Masikini huyu hata umchangie namna gani haridhiki ________________________
(v) Methali ipi inafanana na Haraka haraka haina baraka __________________________________________
5. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata
Tulime jama tulime,tushinde adui njaa,
Hapa kwetu ituhame, kwingine kutokomea,
Wala sisi tusikome, chakula kujilimia,
Tutie embe mpini, tuteremke shambani.
Chakula kujilimia, zaidi kujipatia,
Tuache kutegemea, siku watajigomea,
Siku watajigomea, nani tutakimbilia,
Tutie jembe mpini, tuteremke shambani.
MASWALI
(i) Katika shairi hili mwandishi anazungumzia jambo gani?_________________________________
(ii) Shairi hili lina beti ngapi?_______________________
(iii) Adui mkubwa anaezungumzwa katika shairi hili ni ______________________________
(iv) Vina vya mwisho katika ubeti wa kwanza ni ______________________
(v) Shairi hili lina mizani ngapi ?___________________________________
6. Panga vizuri vipengele vya barua ya kiofisi (kikazi) ili vilete mtiririko mzuri kwa kuzipa
herufi A, B, C, D na E.
(i) Wako mtiifu, HAMADI MPONDA (Mwomba kazi). [ ]
(ii) S.L.P 4212 ARUSHA (Barua itokapo). [ ]
(iii) MKUU WA SHULE CHAWE S.L.P 3010 MBEYA (Barua iendako). [ ]
(iv) YAH: MAOMBI YA NAFASI YA MASOMO. [ ]
(v) TAREHE 10-11-2021. [ ]
HABARI YA KUSIKILIZA
Siku moja Mama mashaka alikuwa anatoka shambani jioni. Walitokea vijana wadogo watatu wakamsalimia kwa
adabu. Mara wakamvamia na kumnyang’anya saa aliyokuwa amevaa, simu yake aina ya Nokia na fedha kiasi cha
shilingi elfu sita. Mama Mashaka alipiga kelele lakini hakukuwa na mtu Jirani wa kumsaidia. Wale vijana
walifanikiwa kukimbia, waliviuza vitu vile na kugawana fedha. Mama Mashaka alimtambua kijana mmoja kati ya
wale watatu ajulikanaye kwa jina la Matatizo. Mama Mashaka alikwenda kwa wazazi wake na kuwaelezea
yaliyojiri. Wazazi wake walisikitika sana, walimwita mtoto wao na kumuuliza alikuwa na kina nani alioshirikiana
nao katika wizi. Matatizo aliwataja Majuto na Mtakahela. Wazazi wake waliwatafuta wote na kuwapeleka ofisi ya
Mtendaji wa Kijiji. Watoto wote watatu wakapewa adhabu ya kufanya usafi kwenye ofisi ya Kijiji kwa mwezi
mzima wakiwa chini ya uangalizi wa kutorudia kosa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA
MTIHANI WA MAJARIBIO DARASA LA SABA
SOMO: MAARIFA YA JAMII
Muda: Saa 1:30 Mwezi Januari, 2025
SEHEMU A: CHAGUZI NYINGI NA VITU VINAVYOFANANA (ALAMA 20)
Chagua herufi ya jibu sahihi na uandike kwenye kisanduku kilichotolewa:
i. Madini yana manufaa kwa mtu mmoja mmoja na taifa. Uchimbaji madini husaidia watu kupata kazi na
malighafi kwa tasnia tofauti. Yafuatayo ni madhara ya uchimbaji madini kwenye mazingira ILA ( )
a) Kusababisha mmomonyoko wa udongo b) Uchafuzi wa hewa c) upandaji miti upya wa mimea
d) magonjwa ya macho e) ugonjwa wa ngozi.
ii. Ni nchi gani kati ya zifuatazo ilikuwa nchi ya kwanza ya kigeni iliyovamia nchi yetu katika karne ya 19?
a) Kireno (b) Oman (c) Uingereza (d) Kifaransa (e) Ubelgiji
iii. Ni istilahi gani kati ya zifuatazo inahusu uharibifu wa mazingira asilia kama vile ardhi, maji, hewa,
mimea na wanyama?a) Uharibifu wa mazingira (b) uchafuzi wa udongo c) uchafuzi wa ardhi
d) Ukataji miti e) upandaji miti.
iv. Je, ni sayari ipi kati ya zifuatazo ambayo ni sayari kubwa zaidi katika mfumo wa jua?( )
a) Zuhura b) Zebaki c) Dunia d) Jupiter e) Mirihi
v. Mwalimu wa Stadi za Ufundi aliwafundisha wanafunzi wake kuhusu mbinu mbalimbali za kupikia.
Akiwa anaeleza Maimuna alinyanyua mkono na kutaka kujua mbinu sahihi za kupika chakula kwa
kutumia maji mengi. Je, unafikiri ni jibu gani sahihi kutoka kwa mwalimu?( )
a. kuoka b. Kuchoma c. Kuchemsha d. Kuchoma e. Kukaanga
vi. Ni vazi gani huvaliwa juu ya mavazi mengine ili kuwalinda watu kama wapishi wasichafuke?( )
a. vifaa vya kichwa b. Kinyago C. Scuff d. Soksi e. Aproni
vii. Je, ni mwendo gani wa Dunia ambapo Dunia inazunguka jua kupitia obiti yake?( )
a) Mapinduzi b) Mzunguko c) Usuluhishi d) Mapinduzi upya e) mzunguko
viii. Njia mbalimbali zinaweza kutumika kuondokana na athari za uharibifu wa mazingira unaosababishwa
na mbinu mbovu. Ni ipi kati ya zifuatazo ambayo sio mazoea mazuri kwenye mazingira?( )
a) Matumizi ya mtaro b) Kulima zao moja c) kubadilisha mazao d) kutumia mbolea za asilia.
e) Kupanda miti katika ardhi tupu
ix. Je, kati ya zifuatazo ni mazoezi gani ya kufuga idadi kubwa ya wanyama katika eneo dogo?( )
a) Kulisha mifugo kupita kiasi b) upandaji miti c) kuacha kufuga wanyama
d) kukatisha tamaa mchungaji e) wingi wa watu
x. Je, ni hatua gani inahitajika kulinda mazingira kutoka kwa eneo la viwanda?( )
a) Kurejeleza taka b) Kutupa g taka c) Kuficha taka d) kuzika taka ardhini
e) Kuzika taka ardhini
xi. Je, kati ya zifuatazo ni kipi kinarejelea mchakato wa malighafi kutumia mashine kuzalisha bidhaa au
bidhaa muhimu? ( )
a) Utengenezaji b) unyonyaji c) usafirishaji nje ya nchi d) Utafutaji
xii. Baraza lenye jukumu la kukuza na kuendeleza kazi ya sanaa asilia ya Tanzania ni ( ).
a) BASATA b) BAKITA c) UKWASI d) TUKI e) TAMWA
xiii. Utamaduni hubainisha na kuunganisha watu wanaoishi katika jamii fulani kupitia vipengele kadhaa
kama vile lugha, chakula, nguo, nyimbo na michezo. Kipi kati ya yafuatayo ambayo pia inaelezewa
kama kipengele cha utamaduni?( )
a) Mila na desturi b) Vita na upendo c) Wanyama na uchumi d) michezo na ukubwa.
e) Masuala ya dini na uhalifu
xiv. Kuna mbinu nne ambazo wanahistoria hutumia kukusanya taarifa kuhusu matukio yaliyopita. Ni ipi
kati ya njia zifuatazo zinazohusisha wanahistoria kutembelea tovuti za kihistoria ambapo
kumbukumbu kuhusu matukio ya zamani zinaweza kupatikana?( )
a) Mahojiano ya mdomo b) c) Uchunguzi wa moja kwa moja
d) Hojaji e) kaboni 14
xv. Bara la Afrika lina waanzilishi wengi waliopinga ukoloni, ambaye alianzisha nchi ya Ghana ni ( )
a) Nelson Mandela b) NKwame Nkurumah c) Patrick Lumumba
d)Samora Machel e) Kamuzu Banda
2.Linganisha kila kipengele kutoka kwenye Safu wima A na vipengee vinavyowiana kutoka kwenye Safu
wima B. Kisha andika herufi ya jibu sahihi katika nafasi iliyotolewa.
Safu wima A Majibu Safu wima b
i.Maeneo ya ustaarabu wa kale A. 1964
ii. Mfumo wa kimwinyi uliokuwepo B. Utafiti wa taasisi za kibinadamu, kijamii au
kando ya maeneo ya pwani ya kitamaduni na uhusiano wao kwa wakati.
Tanganyika
iii. Tanganyika inakuwa Jamuhuri C.Umwinyi
iv. Anthropolojia ya kihistoria D. 1961
v.Muungano wa Tanganyika na E.Olduvai Gorge ya Arusha, Isimila mjini Iringa na
Zanzibar Kondoa Irangi mjini Dodoma.Ushuhuda wa
F. Vyanzo vya habari kuhusu siku za nyuma.
. SEHEMU B: KUJAZA MAPENZI (ALAMA 20)
3.i. Wanafunzi wanashauriwa kutovaa viatu vya kisigino kirefu kwa sababu gani?
a)_____________________________________ b) _________________________________
ii. Mazingira ni muhimu sana katika kusaidia viumbe hai vyote vilivyopo duniani. Mimi hatutunzi mazingira,
maisha yetu yatakuwa hatarini. Taja athari zozote mbili za uharibifu wa mazingira
a)__________________________________________ (b) ____________________________________
iii. …………… ni kifaa kinachotumia mkaa,umeme ,mafuta ya taa ambayo hutumika kufanya nguo zetu
kuonekana nadhifu
4. i.Upepo ni hewa katika mwendo. Upepo unavuma kutoka eneo la _________ hadi eneo la ________
ii.Njia ya kisayansi ya kutabiri hali ya siku hadi siku ya angahewa ambayo imerekodiwa kwa muda mfupi
inaitwa…………………………………………….
iii. Sanduku la mbao ambalo hutumika kuweka kipimajoto na kipima joto huitwa _____________
iv. Ni madini gani hupatikana Tanzania pekee?......................................
5.Utamaduni wa Mtanzania ndio njia kamili ya jinsi watanzania wanavyoishi. Taja umuhimu wowote mbili
wa utamaduni
a) ___________________________ (b) _______________________________
6.Eleza maana ya maneno yafuatayo:
a) Miiko____________________ (b) _______________________
SEHEMU YA C: RAMANI (ALAMA 10)
7. Chunguza mchoro ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata;
Maswali:
(i) Ni mlima gani unaowakilishwa na herufi "A"?
___________________________________
(ii) Jina la kisiwa chenye alama ya herufi "B" ni
nini?
___________________________________
(iii) Njia ya ukabaila iliyofanyika katika eneo
lililowekwa alama ya herufi “E” iliitwa
_______________
(iv) Je, ni njia gani ya uzalishaji inayotekelezwa
katika eneo lililoonyeshwa kwa herufi “C”?
_____________
(v) Taja ishara ya kipengele cha asili
kilichowekwa alama ya herufi “D”
_______________________
MAJIBU
i. C
ii. B
iii. D
iv. C
v. C
vi. E
vii. A
viii. B
ix. D
x. A
xi. A
xii. A
xiii. A
xiv. B
B
2. (I). E
(ii). C
(iii). D
(iv). B
(v). A
3. i. (a). Kuumia misuli
(b). Maumivu ya misuli
ii.
(a). Kupoteza uwezo wa kuzaa na kusababisha mavuno kupungua
(b). Ukame unaoweza kusababisha kifo kwa viumbe hai
iii. pasi
4. i. (a) Shinikizo la juu hadi shinikizo la chini
(b). Utabiri wa hali ya hewa.
ii. (a). Skrini za Stevensoni
iii. (a). Ni ishara ya umoja wa kitaifa na utambulisho wa jamii
(b). Inasaidia jamii kuthamini rasilimali za Taifa
(c). Sisitiza uvaaji wa mavazi ya heshima
(d). Epuka kudhalilisha tamaduni zetu na kuiga za kigeni
iv. Tanzanite
5. (a). Miiko inarejelea mazoea ya kidini au kijamii ambayo yanazuia tabia, shughuli, au
uhusiano fulani
Na watu au vitu.
b). Desturi ni mambo ya kawaida yanayofanywa na wanajamii mara kwa mara
6. (a). Mlima Kilimanjaro
(b). Mafia
(c). Uyarubanja
(d). Uvuvi
(e). Mto Rufiji
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA
MTIHANI WA UPIMAJI
SOMO: SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Muda: Saa 1:30 Januari, 2025
SEHEMU A ( Alama 20)
1. Jibu maswali (i) – (x) kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na uandike kwenye kisanduku
kilichotolewa.
(i) Wanyama wamegawanywa katika makundi makubwa mawili. Ni ipi kati ya zifuatazo inawakilisha wanyama
ambao ni wanyama wasio na uti wa mgongo?____________________( )
(a) Konokono na ngisi (b) ngisi na samaki (c) minyoo na binadamu (d) mjusi na konokono (e) mjusi na ngisi.
(ii) Nyenzo hutumika kwa shughuli mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku ili kurahisisha kazi. Ni ipi kati ya
vifaa vifuatavyo ni mifano ya nyenzo ya daraja la pili? ___________________( )
(a) kopo na toroli (b) koleo na toroli (c) ndoano na koleo la kuvulia Samaki (d) usawa wa chemchemi na mlango
( e) toroli na mlango
(iii) Mafuta ya taa hutiwa katika eneo ambalo mbu huzaliana. Je, kuna umuhimu gani wa kumwaga mafuta?
(a) Kuongeza rutuba kwa mbu (b)Kuondoa harufu mbaya (c)kuzuia oksijeni kuingia kwenye maji ( )
(d) kuua plasmodium (e) kukausha maji.
Rajab alimuuliza baba yake “ni sehemu gani ya kompyuta inatumika kuonyesha picha’ Je, kati ya zifuatazo ni jibu
gani lililo sahihi kutoka kwa baba yake?___________________________( )
(a) spika (b) kibodi (c) kipanya (d) CPU (e) Skrini
v) Mpunga ni zao linalopaswa kulimwa kwenye udongo wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi maji. Ni udongo gani
huo? ______________________________( )
(a) Udongo tifutifu (b) Udongo wa kichanga (c) udongo wa mfinyanzi (d) udongo mwekundu (e) mboji
viNi mnyama gani kati ya wafuatao ni mamalia?_______________( )
(a) panya (b) kuku (c) ndege (d) chura (e) Samaki
vii) Mkondo wa umeme unaotiririka katika saketi ya umeme hupimwa kwa chombo kinachojulikana kama___( )
(a) ohmmita (b) galvanometer (c) ammita (d) voltmeter (e) anemomita
viii) Kama mwanafunzi wa darasa la saba anayekuja ambaye amejifunza vyema kuhusu sifa za viumbe hai, ni
kauli gani kati ya hizi hapa chini ambayo si sahihi kuhusu harakati za viumbe?________________( )
(a) Viumbe vyote vilivyo hai husogea (b) mwendo wa mimea ni polepole sana
(c) kukua pia huhusisha harakati ya mimea (d)Usogeaji wa mmea huhusisha mmea mzima
(e) Mwendo hautokei kwenye mimea.
ix) Ugonjwa wa kurithi ambao hubadilisha umbo la erithrositi kutoka kwa biconcave hadi umbo la nusu mwezi
huitwa___________________________________( )
a) Ualbino (b)Haemophilia (c) Pumu (d)upofu wa rangi (e) anemia ya seli mundu (sickle cell)
x) Kazi zote za kuingiza, kupanga, kuchakata na kutambulisha matokeo hufanywa katika karatasi. ni ipi kati ya
zifuatazo sio aina ya data ya kuingizwa kwenye lahakazi? _______________( )
a) kisanduku (b)maandishi (c)fedha (d) tarehe (e)nambari
2. Oanisha maneno katika sehemu A na sehemu B ilikupata jibu sahihi kwa kuandika herufi ya
jibu sahihi kwenye sehemu ya majibu.
SEHEMU A MAJIBU SEHEMU B
i Magonjwa yanayosababishwa na bacteria A. Kuozesha
ii Ugonjwa wa maumbile unaorithiwa kutoka B. Sickle cell anemia na
kizazi kimoja hadi kingine Haemophilia
iii Bakteria na fangasi C. Poikilothermic
iv Joto la mwili hutofautiana kulingana na joto D. Homoothermic
v la mazingira E. kifua kikuu
Uhusiano kati ya viumbe hai na mazingira F. Kutegemeana
G. Ikolojia
3.Chagua jibu kutoka kwenye kisanduku ili kukamilisha sentensi katika vipengele (i) - (v) kwa makini
kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi iliyotolewa.
Ureta, ateri ya renali, Kuondoa sumu mwilini, veini ya renali, urethra, figo, ini.
i) Hubeba damu iliyochujwa kutoka kwenye figo__________________________________
ii) Kiungo kinachoharibu chembe nyekundu za damu zilizochakaa_______________________
iii) Hutoa mkojo kutoka kwenye kibofu hadi kwenye uume_______________________
iv) Hupeleka damu isiyochujwa hadi kwenye figo ______________________________
v) Ni kiungo kinachochuja damu ___________________________________
SEHEMU B: MAJIBU MAFUPI (alama 20)
Jibu vipengee vyote katika sehemu hii
4. i)Taja hatua mbili za kwanza zilizofuatwa wakati wa kufanya uchunguzi wa kisayansi
a) ______________________________________ (b) _________________________________
ii)Ni sehemu gani kuu mbili za kompyuta __________________________ na ________________________
iii) Mzee Majuto alienda hospitali kupimwa macho na alipewa miwani yenye lenzi mbonyeo. Ni nini lilikuwa tatizo
kwenye macho yake? ____________
5.i) Wavulana na wasichana hupitia mabadiliko tofauti katika hatua ya balehe. Taja njia zozote mbili za kuhimili
mabadiliko yanayotokea wakati wa balehe a) ___________________________________
b) ______________________________
ii) Kabonidayoksaidi + maji + Mwanga wa jua Wanga +oksijeni. Q inawakilisha ________
Q
iii) Mishipa ya damu ni mtandao wa mirija tupu ambayo husafirisha damu katika mwili wote. Jina la mshipa mdogo
zaidi wa damu ni nini? _______________
6. i) Kuna magonjwa mbalimbali ya zinaa, kila moja ina dalili zake kwa wanawake na wanaume. ni ugonjwa gani
wa zinaa unaosababishwa na bakteria waitwao Neiseria? ____________________
ii)Mimea ina umbijani ambayo inachukua nishati ya jua kwa photosynthesis. ni vitu gani vingine vinatumiwa na
mimea kama malighafi? (a) ___________________________ (b) _______________________________
iii )Amani alikatazwa na mama yake kuchezea maji yaliyotuama yenye konokono. Je,mama yake alikua anamkinga
Amani asipate ugonjwa gani?_______________________________________
iv)Ni gesi gani inatumiwa na wanyama kutengeneza protini na pia hutumika kutengeeza mbolea
viwandani?_________________________________________________
SEHEMU C.(Alama 10)
Jibu vipengele vyote katika sehemu hii.
7. Angalia mchoro ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata
a) ______________________________
(b) _________________________
iii) Muunganiko wa gameti wa kiume na wa kike hufanyika
katika sehemu iliyooneshwa kwa namba ngapi? ? ________
8 i) Kokotoa jitihada inayohitajika kunyanyua mzigo wa
gramu 350 kwa kutumia
rodahuru._________________________________________
_________________________________________________
__________________________________
ii) Fundi alitumia nguvu ya 50N kuinua gari. ikiwa kazi
i) Taja jina la sehemu iliyooneshwa kwa namba 2 iliyofanywa ilikuwa 75Joules, Tafuta umbali ambao gari
liliinuliwa. ____________
___________________________________
ii)Orodhesha homoni mbili zinazozalishwa na sehemu
iliyoandikwa 5
MAJIBU.
SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Qns.1
i ii iii iv v vi vii viii ix x
A A D E C A C D E A
Qns.2
i ii iii iv v
E B A C G
3. i.Veini ya ateri.
ii.Ini
iii.Urethra
iv.Ateri ya renali
v.Figo
4.i) a.Kugundua tatizo b)Kubuni dhanio
ii)Maunzi na programu
iii)Kutokuona mbali
5 i) (a)Kufanya mazoezi b) Kula mlo kamili
ii)Umbijani
iii)Kapilari
6.i) Kisonono
ii)Kabonidayoksaidi na maji
iii)Kichocho
iv)Nitrojeni.
7i) Mirija ya Falopia
ii)ostrojeni na progesteroni
iii) 6
8I)175kg
ii)1.5m
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA
MTIHANI WA KUJIPIMA
SOMO: URAIA NA MAADILI
MUDA:Saa 1: 30 Januari, 2025
SEHEMU A: (ALAMA 20)
1. Chagua herufi ya jibu sahihi
i) Ili kujenga familia bora inatupasa kutambua nafasi ya ________________( )
(a) Wazazi tu (b) Watoto peke yake (c) Baba tu d) Kila mwanafamilia (e) Mama tu
ii) Ipi siyo faida ya mwanafunzi kushiriki katika michezo( )
(a) Kujenga mwili na akili (b) Kujenga uhusiano mwema na wengine
(c) Kuleta uhusianiokati ya wanafunzi (d) Kujenga umoja na mshikamano
(e) Kufeli mitihani
(i) Yafuatayo ni makundi ya watu wenye mahitaji maalumu isipokuwa:( )
(a) Watoto wadogo (b) Vijana (c) Wazee
(d) Watoto wadogo (e) Mama wajawazito
(ii) Mambo yanayohusu haki na ustawi wa mtoto yamewekwa kwenye sheria ya mtoto
namba 21 ya mwaka ( )
(a) 2004 (b) 2007 (c) 2009 (d) 2008 (e) 2001
(iii) Kipi kati ya vifuatavyo si kitendo cha heshima? ( )
(a) Kulewa pombe (b) Kusalimia wakubwa (c) Kuvaa kwa staha
(d) Kuwapenda watu wote (e) kuwa na heshima
(iv) Kitendo kipi kati ya hivi vinaweza kujenga tabia hatarishi? ( )
(a) Kucheza kamari (b) Kucheza mpira (c) Kuheshimu watu wote
(d) Kuiga mila na desturi (e ) Kuthamini wenzako
(v) Yafuatayo ni mambo yanayoiletea sifa nzuri shule isipokuwa ( )
(a) Ufaulu wa wanafunzi (b) Mimba za utotoni (c) Nidhamu ya wanafunzi
(d) Mazingira safi ya kujifunza (e) Mwonekano wa mwanafunzi
(vi) Ipi kati ya zifuatayo si mfano wa kauli mbiu ya shule? ( )
(a) Elimu ni rasilimali (b) Ajali haina kinga (c) Nidhamu kwa taaluma bora
(d)Elimu ya ukombozi (e) Elimu ni ufunguo wa maisha
(vii) Chombo kinachozuia na kupambana na rushwa huitwa:-( )
(a) TAKURURU (b) FAO (c) ILO (d) TAKUKURU (e) UNICEFU
(viii) Miongoni mwa mambo yanayowavutia wazazi shuleni ni:( )
(a) Walimu wasiotosheleza shuleni (b) ) Utoro wa wanafunzi (c) ufaulu wa wanafunzi
(d)Uhaba wa nyumba za walimu (e) Mimba za utotoni
2. Oanisha fungu A na fungu B ili kuleta maana sahihi.
FUNGU A MAJIBU FUNGU B
i. Kiongozi bora A. J.K Nyerere
ii. Utii wa sheria B. 1964
iii. Mtoto wa shangazi C. Binamu
iv. Waziri mkuu wa kwanza wa D. Anayesaidia watu kwa
Tanganyika haki
v. Tanganyika na Zanzibar ziliungana E. Ni jukumu la kila raia
F. 1962
3. Tumia maneno yaliyo kwenye kisanduku kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Tarafa, kijiji, wilaya, mkoa, baraza la usuluhishi la kata, halmashauri ya manispaa
(i) Ngazi ndogo ya utawala katika serikali za mitaa __________________________
(ii) Eneo la utawala katika mkoa ambalo ni dogo kuliko mkoa lakini kubwa kuliko tarafa
__________________________________
(i) Eneo la utawala ambalo linajumuhisha wilaya kadhaa _______________________________
(ii) Inahusisha chombo kinachosuluhisha mizozo midogo midogo miongoni mwa wanajamii
___________________________________
(iii) Ngazi ndogo ya utawala katika serikali kuu __________________________________
SEHEMU B: (ALAMA 20)
4. Jaza nafasi ziizoachwa wazi
(i) Jambo linalomlazimu mtu kulifanya au kulitimiza huitwa ___________________
(ii) Ni alama ipi ya taifa inaonyesha uhuru wa nchi __________________________
(iii) Kiongozi washughuli za serikali katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
______________________________________________
(iv) Kati ya mihimili mitatu katika serikali. Je mhimili upi unahusika na utekelezaji wa sheria?
______________________________________________
(v) Kiongozi mkuu wa masuala ya sheria serikalini ni ____________________________
5. Jaza nafasi zilizo wazi
(i) Ushauri nasaha unahitajika ili kuwasaidia wanafunzi kukabiliana na matatizo ya kitaaluma. Tambua
matatizo mawili ya kitaaluma ambayo yanahitaji ushauri nasaha wa kitaaluma kutolewa kwa
wanafunzi.
(a) ________________________________________________________
(b) _______________________________________________________
(ii) Ni taasisi ipi ya serikali inajihusisha na utunzaji wa mazingira? _______________________
(iii) Nani ni mtendaji mkuu wa kamati ya shule? ______________________________
(iv) Ni tukio gani lilifanyika tarehe 10 Desemba 1948? ____________________________
(v) Ni mhimili gani unahusika kutunga sheria za nchi? _____________________________
SEHEMU C: (ALAMA 10)
6. Kielelezo kifuatacho kinawakilisha muundo wa ngazi ya mahakama tanzania. Jaza nafasi zilizo wazi
kukamilisha muundo huo.
MAHAKAMA YA RUFANI
i.
ii.
iii.
iv.
v. Nani ni kiongozi mkuu wa mahakama? ________________________________
MARKING SCHEME
QN 1
i ii iii iv v vi vii viii ix x
D E B C A A B B D C
QN 2
i ii iii iv v
D E C A B
QN3 (i) Village/ kijiji
(ii) District/ Wilaya
(iii) Region/ Mkoa
(iv) Ward tribunal/ Baraza la Usuluhishi kata
(v) Division/ Tarafa
QN4 (i) Responsibility/ majukumu
(ii) National flag/ Bendera ya taifa
(iii) Prime Minister/ Waziri Mkuu
(iv) Executive/ Serikali ya Utendaji
(v) Attorney General/ Mwanasheria Mkuu wa Serikali
QN5 (i) – poor academic performance/ ufaulu hafifu kitaaluma
- Learning difficulties/ changamoto za ujifunzaji
(ii) NEMC
(iii) Head teacher/ Mkuu wa Shule
(iv) Declaration of human rights/ Tamko la haki za binadamu
(v) Parliament/ Bunge
QN6 (i) High court/ Mahakama Kuu
(ii) Resident Magistrate/ Mahakama ya hakimu Mkazi
(iii) District court/ Mahakama ya Wilaya
(iv) Primary court/ Mahakama ya Mwanzo
(v) Chief Justice/ J